Rozari Takatifu (Matendo ya Mwanga) - Alhamisi
1. Ubatizo wa Yesu Mtoni Yordani Wakati huo Yesu akaja kutoka Galilaya mpaka Yordani kwa Yohana ili abatizwe. Naye Yesu alipokwisha kubatizwa mara akapanda kutoka majini; na tazama, mbingu zikamfunukia, akamwona Roho wa Mungu akishuka kama hua, akija juu yake. Na tazama, sauti kutoka Mbinguni ikisema, "Huyu ni mwanangu, mpendwa wangu, ninayependezwa naye." (Mathayo 3:13, 16-17) Ee Mungu, kwa fadhili zako, kwa maji na Roho Mtakatifu, tunazaliwa katika maisha ya uzima wa milele. Tunakusihi kwa wema wako uendelee kuzimimina baraka zako juu yetu; na kutufanya kuwa wana waaminifu wa taifa lako takatifu. Amina. 2. Yesu Ageuza Maji Kuwa Divai Huko Kana Na siku ya tatu palikuwa na harusi huko Kana, mji wa Galilaya; naye mama yake Yesu alikuwapo. Yesu naye alikuwa arusini pamoja na wanafunzi wake. Hata divai ilipowatindikia, mamaye Yesu akamwambia, "Hawana divai." Naye mkuu wa meza alipoyaonja yale maji yaliyopata kuwa divai, alimwita bwana harusi, akamwambia, kila mtu kwanz...